Huyu ndiye mchezaji pekee wa Yanga ambaye hajaungana na wenzake Kambini

Huyu ndiye mchezaji pekee wa Yanga ambaye hajaungana na wenzake Kambini

0

Huyu ndiye mchezaji pekee wa Yanga ambaye hajaungana na wenzake Kambini

Yanga inaendelea na mazoezi ya Kuhakikisha wanakuwa fiti kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika na michezo ya Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara.

Katika Kujiandaa na ligi kuu na mechi za Kimataifa Yanga imeweka kambi mkoani Morogoro na jana ikicheza mechi ya kirafiki na timu ya Tanzanite Academy ambapo Yanga ilishinda bao 5 kwa 1.

Wakati yanga ikiendelea na mazoezi huko Morogoro Mpaka jana ni wachezaji wawili hawakuwa katika kambi hiyo ya Mkoani Morogoro ambao ni Ibraim Ajib Migomba na Mohammed Issa Banka.

Lakini leo asubuhi Ibrahim Ajib ameungana na wenzake katika mazoezi ambapo ameonekana akifanya mazoezi ya peke yake kama Kukimbia uwanja wakati wenzake wakiendelea na Program nyingine.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY