Ishu ya Bilionea Yanga kumvuta Rasta wa Asante Kotoko

Ishu ya Bilionea Yanga kumvuta Rasta wa Asante Kotoko

0

Ishu ya Bilionea Yanga kumvuta Rasta wa Asante Kotoko

Kama kuna wachezaji ambao wamekuwa gumzo siku za karibuni basi ni yule Rasta wa Asante Kotoko ambaye aliisumbua vilivyo safu ya Ulinzi ya Timu ya Simba walipocheza kwenye mchezo maalumu wa Simba Day Agosti 8, 2018.

Taarifa ambazo zimeandikwa na gazeti la Dimba la nchini Tanzania leo zinadai kuwa Kocha Mwinyi Zahera baada ya Kuangalia mchezo ule alivutiwa ipasavyo na Straika huyo Yacouba Songne ambaye ni raia wa Burkinafaso.

Baada ya Kuvutiwa na uwezo wa Straika huyo kocha huyo kulingana na Taarifa hiyo ameshalifikisha jina la Straika huyo Rasta wa Asante Kotoko Yacouba Songne kwa  bilionea  mmoja wa Yanga ambaye anatajwa ndiye aliyefanikisha usajili ya Papy Kabamba Tshishimbi kutua Yanga.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY