Ishu ya Shubhash Patel kumrithi Manji Yanga hii hapa

Ishu ya Shubhash Patel kumrithi Manji Yanga hii hapa

0

Ishu ya Shubhash Patel kumrithi Manji Yanga hii hapa

Wakati baadhi ya wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wakiamini kuwa Yusuph Manji atarejea Yanga baadhi wameonekana kukata tamaa juu ya Kurejea kwa Yusuph Manji kama mwenyekiti wa timu hiyo.

Kutokana na hali hiyo kuna Taarifa kutoka gazeti la Jangwani ambalo huandika habari nyingi za Yanga kuwa baadhi ya wanachama kwasasa wanajipanga kumshawishi mfanyabiashara mwenye pesa zake Shubhash Patel  kumrithi Yusuph MANJI.

Taarifa hiyo inadai wanachama hao wanaamini inawezekana ikawa rahisi kwa Shubhash Patel kuwekeza Yanga kama timu hiyo itafanya uchaguzi na kupata viongozi wapya hali ambayo inaweza ikavutia wawekezaji wengi zaidi kama Shubhash Patel ambaye amewahi kutangaza biashara zake kupitia jezi za Yanga zamani.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY