Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Rayon Sports 29.8.2018

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Rayon Sports 29.8.2018

0

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Rayon Sports 29.8.2018

Leo kutakuwa na Mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF mchezo wa Kundi D kati ya Rayon Sports dhidi ya Yanga ya nchini tanzania Mechi ikichezwa jijini Kigali katika uwanja wa Nyamirambo.

Kulingana na Kikosi cha Yanga kilichoenda Kigali rwanda hiki ndicho Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza leo mbele ya Rayon Sports.

Golini : Ni wazi kipa Beno kakolanya ataanza langoni kutokana na uimara ambao amekuwa akiuonyesha anapokuwa langoni kiasi cha Kumfanya kuaminika kimataifa na hata kwenye mechi za Ligi Kuu.

Mabeki wa pembeni : Kidogo Yanga leo inachangamoto na nafasi ya Ulinzi wa Kulia kutokana na Juma Abdul kuwa majeruhi na hakuna mchezaji katika Kikosi cha Yanga ambaye anaasili ya Kucheza kama beki wa Kulia baada ya Kuondoka Hassan Kessy

Lakini msomaji wa Kwataunit.co.ke navyoangalia Kikosi cha Yanga leo Kulia anaweza akaanza Vicent Andrew ambaye amewahi kucheza nafasi kama hiyo akiwa Mtibwa Sugar huku shavu la Kushoto kama kawa kama dawa Gadiel Michael.

Mabeki wa Kati : Kelvin Yondani ” Cotton Juice” anaweza akasimama na Abdallah Shaibu Ninja.

Viungo namba 6 na 8 : Hapa leo kunaweza kuwa na mabadiliko kutokana na Kukosekana kwa mtu kama Tshishimbi kwahiyo naiona nafasi ya Raphael Daud akianza na Pius Buswita katika eneo la Kati ya uwanja.

 

Viungo wa Pembeni : Namba 7 na 11 Hapa Deus Kaseke kama namba 11 na NAMBA 7 Yusuph Mhilu anaweza akarejea kwenye Kikosi leo  au Buswita akacheza kama kiungo wa Pembeni na Kisha katikati akanza pato Ngonyani ili kuimarisha zaidi ulinzi

Washambuliaji : Namba 9 Heritier Makambo anaweza akasimama na matheo Anthony ambaye aliongezwa katika wachezaji watau kwenye Kikosi cha Yanga. Kukipata kikosi chenyewe kwa wakati Hakikisha umelike Ukurasa wetu wa Facebook, Bonyeza HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY