Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya USM Alger leo 19.8.2018

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya USM Alger leo 19.8.2018

0

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya USM Alger leo 19.8.2018

Kikosi cha Yanga leo kinashuka dimbani kucheza dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF.

Hiki ni Kikosi cha Utabiri ambacho kinaweza kuanza leo dhidi ya USM Alger.

Golini : Golikipa Beno Kakolanya anaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kusimama kama mlinda mlango wa Yanga kwa siku ya leo sababu upinzani pekee ambao anaweza kuupata ni kutoka kwa Ramadhan Kabwili.

Mabeki wa Kulia na Kushoto : Namba mbili Juma Abdul ambaye ni kama hana mpinzani kwasasa mara baada ya Hassan Kessy kuondoka Yanga huku namba tatu Gadiel Michael anaweza kuanza kwenye mchezo wa Leo.

Mabeki wa Kati, Namba nne na Tano – Andrew Vincent Chikupe “Dante” na Kelvin Yondani wanaweza kutengeneza pacha leo hii kama mabeki wa Kati kwani mara nyingi wanaelewana tofauti na mmojawapo anapocheza na Mtu kama Abdallah Shaibu.

Viungo wa Kati : Namba 6 na 8 Kwenye mchezo wa Yanga na Mawenzi kocha wa Yanga alimwanzisha Abdallah Shaibu kama namba 6 na Tshishimbi kama namba 8 lakini kocha Mwinyi Zahera anaweza kufanya hivyo pia leo au akaamua kumwanzisha Tshishimbi na Buswita au kamusoko katikati.

Viungo wa Pembeni – Namba 7 na 11 Hapa naona nafasi ya moja kwa moja kwa Deus Kaseke kama namba 11 Na Namba 7 Juma Mahadhi.

Bonyeza hapa KULike Ukurasa wetu wa facebook kuzipata habari kwa Haraka zaidi

Washambuliaji : Namba 9 na 10  msomaji wa Kwataunit Hapa naona nafasi ya Heritier Makambo kama namba 9 na namba 10 mchezaji ambaye amekuwa akiaminika zaidi na Kocha mwinyi zahera Matheo Anthony.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY