Kipa mpya wa Yanga amgomea Kichuya kwenye hili

Kipa mpya wa Yanga amgomea Kichuya kwenye hili

0

Kipa mpya wa Yanga amgomea Kichuya kwenye hili

Wakati Ligi kuu Tanzania bara ikiwa ipo njiani kabisa na ikiwa zimesalia siku sita kitimtim kianze kipa wa Yanga Klaus Kindoki ameanza tambo kuelekea mechi za Ligi kuu.

Klaus Kindoki ambaye ameingia Yanga kuchukua nafasi ya Mcameron Youthe Rostand ambaye alisitishiwa mkataba wake amemtambia Kichuya asahau kumfunga kama alivyokuwa akiwafunga makipa wengine wa Yanga kwa magoli ya Krosi na Kona.

Mpaka sasa Shiza Kichuya ameshawafunga makipa wa Yanga karibu wote ambao wamewahi kucheza na yeye akiwa ndani ya kikosi katika mechi za watani wa Jadi ukianzia na Ally Mustapha ambaye alifungwa goli la Kona.

Deogratius Munishi Dida ambaye alifungwa goli la Mpira wa Nje ya Kumi na nane uliopigwa kwa kwa style kama ya Banana Chop na Youthe Rostand mpira uliopigwa na Kichuya Kumalizia kazi.

Bonyeza hapa KULike Ukurasa wetu wa facebook kuzipata habari kwa Haraka zaidi

Kutokana na hayo msomaji wa Kwataunit.co.ke  Klaus Kindoki amefunguka kuwa Kichuya na wachezaji wanaotegemea kuwafunga Yanga kwa aina ya magoli ya kona na Krosi basi wasahau kwani amejipanga ipasavyo na kipa yoyote mzuri ni lazima aweze kucheza mipira ya namna hiyo katika kiwango cha Juu.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY