Kocha Simba apagawa na Mchezaji wa Asante Kotoko azungumzia Kumsajili

Kocha Simba apagawa na Mchezaji wa Asante Kotoko azungumzia Kumsajili

0

Kocha Simba apagawa na Mchezaji wa Asante Kotoko azungumzia Kumsajili

Hakika siku ya Jumatano 8.8.2018 ilikuwa moja kati ya Siku bora zaidi kwa Simba kwa Mwaka huu kwani licha ya Kufanya mambo mengi kama Klabu ikiwemo kutambulisha Timu zao za Vijana na ile ya wanawake na timu kubwa Ya Simba walipata nafasi ya Kucheza na Moja ya Timu bora kabisa barani Afrika.

Katika mechi hiyo msomaji wa Kwataunit.co.ke ilishuhudiwa Simba ikimaliza mchezo kwa kubanwa kwa sare ya bao 1 kwa 1 bao la Simba likifungwa na Emmanuel Okwi.

KOCHA APAGAWA NA RASTA WA ASANTE KOTOKO.

Wakati watu wengi walioshuhudia mechi hiyo wakipagawa na uwezo wa Rasta wa Asante Kotoko kumbe hata kocha wa Simba Patrick Aussems naye alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wakivutiwa naye kutokana na Kuichachafya Vilivyo safu ya Ulinzi ya Simba.

Magazeti ya Michezo leo 10.8.2018

Mchezaji mwenyewe ambaye wengi walimkariri kutokana na RASTA zake anaitwa Yacouba Songne ambaye licha ya Kucheza Asante Kotoko ya Ghana lakini ni raia wa Burkinafaso.

Kocha wa Simba Patrick Aussems raia wa Ubelgiji akizungumza baada ya Mchezo huo ameweka wazi kuvutiwa kwake na STRAIKA huyo na kusema kuwa kama atahitaji straika wakati wa dirisha dogo basi chaguo lake la kwanza litakuwa ni mchezaji huyo Yacouba Songne kutoka Asante Kotoko wazee wa Kumasi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY