Kocha Simba : Siumii na matokeo ya sare nayoyapata

Kocha Simba : Siumii na matokeo ya sare nayoyapata

0

Kocha Simba : Siumii na matokeo ya sare nayoyapata

Kama unafikiri kocha wa Simba Mbelgiji Patrick Aussems anachukizwa na matokeo anayoyapata kwasasa basi utakuwa unajidanganya mwenyewe.

Kocha huyo wala matokeo ya sare dhidi ya Asante Kotoko na hata matokeo ya sare dhidi ya timu ya daraja la kwanza ya Namungo Fc wala hayamuumizi kicha.

Sikia sasa Kocha mbelgiji wa Simba amefunguka kuwa Matokeo anayoyapata kwasasa hayamsumbui kichwa na anachokifanya kwenye mechi za kirafiki ni kujaribu wachezaji wake na mifumo mbalimbali na watu wakitaka matokeo ya ushindi wasubiri kwenye mechi za Ligi Kuu.

Ila kwasasa bado anasuka Kikosi chake ili kujua ni mchezaji gani amtumie na kwa wakati gani ndiyo maana katika michezo ya kirafiki amekuwa akijitahidi kuwapa wachezaji wengi nafasi ya kucheza hivyo hafikirii sana juu ya Matokeo anayoyapata kwasasa.

AFUNGUKA KUELEKEA MCHEZO WA MTIBWA SUGAR NGAO YA JAMII

Kocha Patrick Aussems amefunguka kuwa mchezo huo ni muhimu sana kwao na moja ya mikakati yake ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo muhimu unaokuwa mbele yao na kutwaa kila taji ambalo Simba itakuwa inashiriki.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY