Kocha Zahera aanza kuchekelea baada ya Hili Yanga

Kocha Zahera aanza kuchekelea baada ya Hili Yanga

0

Kocha Zahera aanza kuchekelea baada ya Hili Yanga

Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Mwinyi Zahera ameanza kuchekelea mwenyewe juu ya Kile ambacho anakiona kwenye kambi ya Yanga huko mkoani Morogoro.

Kocha Mwinyi Zahera amefunguka kuwa anafurahishwa sana na maendeleo ya Kikosi chake na Kusema anaona mabadiliko makubwa sana tofauti na awali kabla hawajacheza na Gor Mahia.

Mwinyi Zahera ambaye ni raia wa Congo amefunguka kuwa kama viongozi wa Yanga wangeweka kambi Morogoro kabla ya Kucheza na Gor Mahia basi anauhakika wangewashinda mechi zote mbili.

KINACHOMFURAHISHA ZAIDI KAMBI YA MOROGORO.

Kocha Mwinyi Zahera amesema anafurahishwa na kambi hiyo kwani wachezaji wanakula Vizuri na kupata muda mwingi wa Kupumzika hali inayowafanya kuonekana kufanya vizuri hata mazoezini na kumpa matumaini ya kufanya vyema kwenye ligi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY