Maamuzi ya Kocha wa Stars baada ya kukutana na wachezaji wa Simba...

Maamuzi ya Kocha wa Stars baada ya kukutana na wachezaji wa Simba aliowatema

0

Maamuzi ya Kocha wa Stars baada ya kukutana na wachezaji wa Simba aliowatema

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike amekutana na kuzungumza na nyota wa Simba aliowatema kwenye kikosi chake baada ya kuchelewa kuripoti kambini. .
.
Baada ya mazungumzo hayo TFF kupitia msemaji wake Clifford Ndimbo imetoa taarifa kuwa suala hilo limekwisha na kwamba hakuna kitakachozuia nyota hao kuitwa tena Taifa Stars kama tu wataonyesha kiwango kizuri kwenye klabu yao.

Hata hivyo, nyota hao wataukosa mchezo dhidi ya Uganda kwavile tayari nafasi zao zimejazwa na wachezaji wengine.

Kwa upande wa msemaji wa Simba, Haji manara amewaomba mashabiki wote wa klabu hiyo kuisapoti timu ya taifa kwa nguvu zote kwani baada ya kikao hicho jambo hilo limekwisha na hakuna mwenye kinyongo, si wachezaji, kocha wala TFF.

CREDIT : Boiplus Media

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY