Maamuzi ya Mwisho waliyokubaliana Yanga na Rostand haya hapa

Maamuzi ya Mwisho waliyokubaliana Yanga na Rostand haya hapa

0

Maamuzi ya Mwisho waliyokubaliana Yanga na Rostand haya hapa

Moja kati ya wachezaji ambao wamekuwa wakipewa lawama nyingi na washabiki basi bila shaka ni Youthe Rostand washabiki wengi wakiamini kipa huyo amekuwa akifungwa magoli mengine kwa uzembe wake binafsi.

Hata upande wa benchi la Ufundi kupitia kwa Kocha wake Mwinyi Zahera imewahi kuelezwa kuwa haridhishwi sana na uwezo wa Rostand ndiyo maana akaletwa Kipa Mkongo Klaus Kindoki.

Awali ilielezwa kuwa Yanga ingemtoa kwa Mkopo Youthe Rostand kwenda African lyon lakini suala hilo lilishindikana dakika za Mwisho kabisa baada ya Lyon kushindwa kuelewana na Yanga kwenye suala la kumlipa Mshahara Youthe Rostand, Kwani Rostand alikuwa anatakiwa kulipwa Mshahara kama wa Yanga kiasi cha milioni 2.7 kwa mwezi wakati Lyon dau lao lilikuwa kama shilingi laki 7 pekee.

Baada ya hayo yote inaelezwa Yanga wameshakaa na Youthe Rostand na wamekubaliana kuvunja mkataba na sasa atalipwa kiasi cha shilingi milioni 25 ili kuvunja mkataba huo.

Milioni hizo 25 ni milioni 8.1 mishahara ya miezi mitatu ambayo Youthe Rostand anaidai Yanga na milioni nyingine 17 ambazo zipo kwenye kipengele cha Kuvunja Mkataba kati ya Klabu ya Yanga na Kipa Huyo raia wa Cameron Aliyejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea timu ya AFrican Lyon.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY