Masoud Djuma na Kocha Mpya Aussems watofautiana kwenye Hili

Masoud Djuma na Kocha Mpya Aussems watofautiana kwenye Hili

0

Masoud Djuma na Kocha Mpya Aussems watofautiana kwenye Hili

Simba kwasasa ipo nchini Uturuki ikiwa inajiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, Mchezo dhidi ya Asante Kotoko siku ya Simba day 8.8.2018 mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa CCM Kirumba Mwanza na Mashindano mengine yaliyo mbele yao.

Wakati Simba inajiandaa na mambo hayo ikumbukwe kuwa Kocha Masoud Djuma ndiye kocha ambaye amekuwa na Timu kabla ya kuja kwa kocha mpya Patrick Aussems ambaye ni raia wa Ubelgiji.

Masoud PIA mara kadhaa aliachiwa timu ya Simba kipindi akiwa na Kocha Mkuu Mcameron Omog lakini pia baada ya mkataba wa Pierre Lechantre kumalizika huku toka atue Simba Masoud Djuma amekuwa muumini wa mfumo wake wa Uchezaji.

Masoud Djuma Msomaji wa Kwataunit.co.ke amekuwa muumini wa MFUMO wa 3,5,2 na mara zote amekuwa akitumia mfumo huo toka kocha Omog alipoondoka Simba na Timu kubaki nayo yeye.

Na hata alipokuja kocha Pierre Lechantre aliendelea kutumia mfumo wa Kocha Masoud Djuma wa 2,5,2.

Lakini kocha Mpya wa Simba Patrick Aussems ameonekana kutofautiana na mfumo huo pendwa wa Masoud Djuma kwani kocha huyo ameonekana kutumia mifumo tofauti.

Mazoezi ambayo yanaendelea nchini Uturuki kocha Mpya Patrick Aussems amekuwa akitumia mfumo wa 4,4,2 na mara nyingine amekuwa akitumia mfumo wa 4,3,3 na hata katika mchezo wa jana wa Kirafiki alitumia 4,4,2.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY