Matokeo Arusha United vs Simba leo 15.8.2018

Matokeo Arusha United vs Simba leo 15.8.2018

0

Matokeo Arusha United vs Simba leo 15.8.2018

Matokeo mechi ya kirafiki kati ya Arusha United ( Zamani JKT Oljoro ) wakicheza dhidi ya mabingwa wa soka Tanzania Bara klabu ya Simba

Timu zote zipo uwanjani na Muda wowote mechi itaanza

Arusha United ndiyo watakaoanzisha Mpira

Mechi imeanza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib

Arusha United 0 – 0 Simba

Dakika ya 5, Matokeo Arusha United vs Simba

Arusha United 0 – 0 Simba

Goaaaaaaaaaal Emmanuel Okwi katika dakika ya sita anakwamisha mpira Nyavuni baada ya Kumpindua beki na Kisha kumtungua Kipa

Dakika ya 12 Simba wanapata Kona, Hassan Dilunga anapiga Kona Okwi anapiga mpira kwa Kichwa Unapaa

Goaaaaaaaaaal Dakika ya 17 Ally Salum Kabunda anasawazisha bao kwa timu yake ya Arusha United baada ya mabeki wa Simba kushindwa kuondoa mpira kwa wakati

Arusha United 1 – 1 Simba

Dakika ya 24 Emmanuel Okwi anawakosa goli Arusha United mpira unagonga Besela

Goaaaaaal Emmanuel Okwi kwa mara nyingine anawainua washabiki wa Simba

Arusha United 1 – 2 Simba

Dakika ya 34 Mkude anachapa shuti kali mpira unagonga Mwamba wa chini na Kurudi Uwanjani

Dakika ya 43 Hassan Dilunga anaonekana Kuumia na anashindwa kuendelea na pambano mwenyewe anaomba afanyiwe mabadiliko.

Dakika ya 45 Cletous Chama anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga

Baada ya Kuingia Chama mashabiki wengi wa Simba wameshangilia kwa Nguvu

Mpira kwa sasa ni Mapumziko

Arusha United 1 – 2 Simba

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha pili kimeanza.

Dakika ya 48 Chama anajaribu Shuti langoni mwa Arusha United Mpira Unapaa juu

Dakika ya 50 Simba wanakosa bao jingine la Wazi kabisa Chama anatoa pasi ambayo kipa anaiona na Kuidaka kabla haujafika kwa Okwi

Dakika ya 56 Simba wanafanya mabadiliko kwa Kumtoa James Kotei na nafasi yake inachukuliwa na Mohammed Rashid “T Better”

Dakika ya 50 sasa Mpira ukionekana kumilikiwa zaidi na Timu ya Simba inayoongoza kwa Magoli

Arusha United 1 – 2 Simba

Dakika ya 72 Adam Salamba anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya Meddie Kagere

Dakika ya 80 anatoka Emmanuel Okwi anaingia Rashid Juma, Bado Arusha 1 – 2 Simba

Dakika ya 85 Simba bado wanaongoza kwa bao 2 kwa 1 Magoli ya EmmanueL Okwi

FULL TIME 

Arusha United 1 – 2 Simba Sc (Kabunda, – Emmanuel Okwi magoli yote)

Matokeo Mkamba Rangers vs Yanga

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY