Matokeo Simba vs Mbeya City TPL Leo 27.8.2018

Matokeo Simba vs Mbeya City TPL Leo 27.8.2018

0

Matokeo Simba vs Mbeya City TPL Leo 27.8.2018

Matokeo ya Moja kwa moja kati ya Simba dhidi ya Mbeya City kutoka Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Mechi Imeanza

Dakika ya kwanza Simba wanapata Kona

Inapigwa Kona lakini inashindwa kuzaa matunda

Dakika ya 2

Simba 0 – 0 Mbeya City

Dakika tano za Awali Simba wanaonekana kutawala pambano huku mbeya City wakionekana kupaki Basi , BADO ni 0 kwa 0

Goaaaaaaal Meddie Kagere anaipatia Simba goli kwa Diving Header baada ya Kupenyezewa Mpira na Shiza Kichuya

Simba 1 – 0 Mbeya City

Baada ya Kufungwa bao Mbeya City nao wanaonekana kuanza kufunguka na Kutengeneza mashambulizi kadhaa, Bado Simba 1 Mbeya City 0 Bao la Meddie Kagere

Dakika ya 20

Simba 1 – 0 Mbeya City

Dakika ya 26 Mbeya City wanafanya Shambuzi la Kiume langoni mwa Simba, Zinatokea Piga nI kUPIGE na kupelekea Aishi Manula Kuomba msaada baada ya Kuumia wakati Wa Shambulizi

Dakika 30 zimekatika uwanja wa Taifa jijini Dar Es SaLaam matokeo bado yakiwa Simba 1  na Mbeya City 0.

Dakika ya 35

Simba 1 – 0 Mbeya City ( Goli la Meddie Kagere)

Dakika ya 43 Mchezaji wa Simba Meddie Kagere anapewa kadi ya njano baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Mbeya City Eric Kyaruzi

Goaaaaaaaaal Yule yule Meddie Kagere dakika ya 45 anachumpa kichwa Kichwa kingine, Diving header kutoka kwa pasi ya Asante Kwasi

Simba 2 – 0 Mbeya City

HALF TIME

Simba 2 – 0 Mbeya City (Yote ya Meddie Kagere)

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha Pili kimeanza

Simba 2 – 0 Mbeya City

Golikipa Aishi Manula anashindwa kuendelea na mpira baada ya Kuumia toka kipindi cha Kwanza na nafasi yake inachukuliwa na Kipa Ali Salim ambaye hii inakuwa mechi yake ya Kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara TPL.

Dakika ya 60 Simba wanafanya Shambulizi lingine la Kiume Langoni mwa Mbeya City lakini Beki wa City anaokoa Shujaa mpira ambao John Bocco angeugusa lingekuwa Bao.

Dakika ya 70 Simba wanapata Kona, Inapigwa lakini Meddie Kagere anacheza faulo

Dakika ya 72 Simba wanafanya mabadiliko kwa kumtoa Hassan Dilunga na Nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla

Dakika ya 70 Peter Mapunda anajaribu shuti kali Ali Salim anautoa na Kuwa kona

Simba 2 – 0 Mbeya City

Dakika ya 83 anaingia Adam Salamba anatoka John Bocco

Dakika ya 88 Eliud Ambokile anaachia mkwaju langoni mwa Simba, Kipa Salim anakuwa shujaa, anautoa na Kuwa kona

Simba 2 – 0 Mbeya City

FULL TIME

Simba 2 – 0 Mbeya City (Mabao ya Meddie Kagere)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY