Matokeo Simba vs Mtibwa Ngao ya Jamii 18.8.2018

Matokeo Simba vs Mtibwa Ngao ya Jamii 18.8.2018

0

Matokeo Simba vs Mtibwa Ngao ya Jamii 18.8.2018

Matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Simba na Mtibwa Sugar Ngao ya Jamii 18.8.2018 uwanja wa CCM KIRUMBA wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Timu zote ziko uwanjani na Wallace Karia Rais wa TFF ndiye mgeni rasmi na Yupo anazikagua

Mechi Imeanza kati ya Simba na Mtibwa Sugar uwanja wa CCM KIRUMBA

Simba 0 – 0 Mtibwa

Dakika ya 1 Tu Simba wanaanza kwa kufanya shambulizi langoni mwa Mtibwa lakini inakuwa Goal Kick .

Dakika ya sIMBA wanapata kona inayochongwa na Hassan Dilunga

Dilunga anapiga Kona Fupi inaungwa kipa Tinocco anadaka

Dakika ya 4 Mtibwa Sugar wanapata Kona, Inapigwa na Issa Rashid Baba Ubaya, Aishi Manula anaudaka

Wakati walinzi wa Mtibwa wakimuacha acha Emmanuel Okwi anajaribu shuti la Nje ya 18 mpira Unagonga mwamba  wa Juu unatoka Nje

Dakika ya 11 Hassan Dilunga anajaribu shuti la nje ya 18 mpira unatoka nje ya Lango.

Dakika ya 15

Simba 0 – 0 Mtibwa Sugar

Mpaka sasa bado mechi ni ngumu kwa pande zote hakuna timu ambayo imeshapata matokeo

Dakika ya 20

Simba 0 – 0 Mtibwa

Dakika ya 22 Awadh Juma anapiga shuti kali Aishi Manula anaubabatiza na kuwa Kona.

Goaaaaaaaal Meddie Kagere anaipatia Simba bao la Kwanza

Simba 1 – 0 Mtibwa

Goaaaaaaaaaaal Kelvin Sabato Kiduku anasawazisha kwa shuti kali baada ya kupenyezewa mpira mzuri.

Simba 1 – 1 Mtibwa

Dakika ya 34 Kelvin Sabato anajaribu tena mpira unagonga mwamba wa Juu. Sabato kacharuka

DAKIKA YA 40

Simba 1 – 1 Mtibwa Sugar

Dakika ya 45 Hassan Dilunga ambaye alitokea Mtibwa anaifungia Simba bao la Pili, Baada ya Kufunga anawaomba msamaha washabiki wa Mtibwa Sugar

HALF TIME

Simba 2 – 1 Mtibwa Sugar (Kagere, Dilunga – Kelvin Kiduku)

Bonyeza hapa KULike Ukurasa wetu wa facebook kuzipata habari kwa Haraka zaidi

KIPINDI CHA PILI

Mtibwa wanaanza kwa kasi na Kupata Kona dakika ya 46

Simba 2 – 1 Mtibwa

Dakika ya 50

Simba 2 – 1 Mtibwa

Dakika ya 54 Mtibwa Sugar wanapata kona Inapigwa Manula Aishi anatoa na mabeki wanaokoa zaidi.

Dakika 60 zimeshakatika Matokeo yakiwa bado 2 kwa Simba na 1 Kwa Mtibwa Sugar

Dakika ya 63 Juma Luizio wa Mtibwa anaingia kuchukua nafasi ya Awadh Juma, Wote hawa wamewahi kucheza Simba

Dakika ya 65 Okwi anaonekana kuumia na huenda akashindwa kuendelea na mchezo

Dakika ya 66 John Bocco anaingia kuchukua nafasi ya Emmanuel Okwi

Dakika ya 73 Shiza Kichuya Anatoka anaingia Shomari Kapombe

Dakika ya 75

Simba 2 – 1 Mtibwa

Dakika ya 77 Simba wanapata faulo ndani ya 18 baada ya Kipa wa Mtibwa Kudaka mpira aliorudishiwa na mchezaji wake

Dakika ya 78 Mzamiru Yassin anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga.

Simba 2 – 1 Mtibwa

Dakika ya  83 Saleh Hamis anatoka anaingia Ally Makalani upande wa Mtibwa Sugar

Dakika 4 za Nyongeza

Simba 2 – 1 Mtibwa Sugar (Kagere, Dilunga – Kelvin Kiduku)

FULL TIME

Simba 2 – 1 Mtibwa

Bonyeza hapa KULike Ukurasa wetu wa facebook kuzipata habari kwa Haraka zaidi

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY