Mawenzi Market vs Yanga leo 12.8.2018 Morogoro

Mawenzi Market vs Yanga leo 12.8.2018 Morogoro

0

Mawenzi Market vs Yanga leo 12.8.2018 Morogoro

Klabu ya Yanga leo itakuwa na Shughuli kadhaa lakini lengo kubwa ikiwa ni kumuaga nahodha wa muda mrefu wa timu hiyo Nadir Haroub Cannavaro ambaye alijiunga na Yanga akitokea Malindi ya Zanzibar.

Katika mkakati huo Yanga itacheza mchezo maalum wa Kumuaga Nadir Haroub Cannavaro na timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza Mawenzi Market ya mkoani Morogoro KATIKA uwanja wa Jamhuri kuanzia saa kumi alasiri

Lakini itakuwa nafasi nyingine kwa wana Yanga kuweza kushuhudia wachezaji wake wapya ambao  baadhi ya wachezaji hao wanasikia tu juu ya uwezo wao lakini bado hawajawaona wakifanya Yao.

Wachezaji kama Kipa Klaus Kindoki na Heritier Makambo ni mojas ya wachezaji wanaosubiriwa kwa hamu kubwa na washabiki na wapenzi wa Yanga.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY