Mechi ya simba dhidi ya Mbeya City yasogezwa mbele

Mechi ya simba dhidi ya Mbeya City yasogezwa mbele

0

Mechi ya simba dhidi ya Mbeya City yasogezwa mbele

 

Bodi ya ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPLB imefanya mabadiliko ya mchezo kati ya Simba na Mbeya City mchezo ambao awali ulipangwa uchezwe jumamosi 25 Agosti 2018.

Mchezo huo sasa utachezwa Jumatatu 27 Agosti 2018 katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuanzia majira ya saa kumi na mbili Jioni.

Simba itakutana na Mbeya City ambao jana walianza kwa Kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam Fc kwa bao mbili kwa 0 wakati Simba ikianza kwa Ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Tanzania Prisons.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY