Muda wa mechi kati ya Simba na Wamorocco leo 1.8.2018

Muda wa mechi kati ya Simba na Wamorocco leo 1.8.2018

0

Muda wa mechi kati ya Simba na Wamorocco leo 1.8.2018

Baada ya mazoezi ya takribani wiki mbili na siku mbili Klabu ya Simba ikijifua vilivyo huko nchini Uturuki leo Klabu ya Simba itashuka dimbani kucheza mchezo wa Kirafiki na klabu kutoka Nchini Morocco anakokipiga Mtanzania Simon Msuva.

Magazeti ya Michezo leo

Simba itacheza na Klabu ya Mouloudia Oujda ambayo ndiyo Mabingwa wa Ligi daraja la Kwanza kwa msimu uliopita na wamepanda daraja mpaka ligi kuu kwenye msimu wa 2018/2019.

Simba itashuka kucheza mchezo huo majira ya saa kumi kamili alasiri kwa saa za AFRIKA Mashariki mchezo  unaosubiriwa na washabiki wengi wa Simba ili kuona Kocha wao mpya atapanga vipi kikosi chao lakini pia KIWANGO cha timu yao.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY