Ratiba Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara TPL Leo 25.8.2018

Ratiba Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara TPL Leo 25.8.2018

0

Ratiba Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara TPL Leo 25.8.2018

Ligi Kuu soka ya Tanzani bara inaendelea leo baada ya mechi za Raundi ya Kwanza kukamilika kwa mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Mbeya City Alhamisi usiku.

Leo  Agosti 25 2018 kutakuwa na Mechi takribani 4 zitakazochezwa katika nyasi za Viwanja mbalimbali Tanzania Bara

Singida vs Mwadui

Katika uwanja wa Namfua kutakuwa na Mechi kati ya Singida United watakaokuwa wenyeji wa Mwadui Fc kutoka wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga. Mechi itaanza saa nane mchana

Coastal Union vs Biashara United

Katika uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga kutakuwa na mchezo kati ya Coastal Union watakaowakaribisha wageni katika Ligi Biashara United ya Mkoani Mara. Mechi hii msomaji wa Kwataunit.co.ke itaanza saa nane mchana

Msimamo Ligi KUU Tanzania bara TPL 2018/2019

Mtibwa Sugar ambao wametoka kupokea kichapo kutoka kwa Yanga watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro Prisons  waliotoka Kupokea Kichapo kutoka kwa Simba. Mechi saa kumi alasiri.

Nako katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni  jijini Dar es Salaam JKT Tanzania  ambao walianza ligi kuu kwa kutoa sare wakicheza na KMC ya Kinondoni watakuwa wenyeji wa Lipuli Fc wanaPaluhengo kutoka Iringa . Mechi itapigwa saa kumi kamili alasiri.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY