Ratiba ligi kuu Tanzania bara TPL 26.8.2018

Ratiba ligi kuu Tanzania bara TPL 26.8.2018

0

Ratiba ligi kuu Tanzania bara TPL 26.8.2018

Ligi Kuu soka ya tanzania bara maarufu kama TPL itaendelea leo kwa mechi 4 kuchezwa zikiwemo baadhi ya mechi ambazo zilitakiwa kuchezwa jana.

Mechi za Leo ligi kuu soka ya Tanzania bara zitakuwa ni kati ya Mtibwa na Prisons mechi ikichezwa mkoani Morogoro katika nyasi za uwanja wa Manungu.

Mechi nyingine msomaji wa Kwataunit.co.ke itakuwa ni kati ya wazee wa Mpapaso Ruvu Shooting ambao mechi iliyopita walilala mbele ya Ndanda Fc wanakuchele, Leo Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa KMC katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Nao chama la wana waite Stand United wapiga debe hawa kutoka mkoani Shinyanga watakuwa wenyeji wa Mbao Fc timu zote zikishinda mechi zao za awali TPL 2018/2019.

Na JKT Tanzania baada ya kuanza kwa sare TPL 2018/2019 leo watakuwa wakiwakariisha wajukuu wa Chief Mkwawa Lipuli wanapaluhengo kutoka Iringa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni jijini Dar Es Salaam.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY