Sheria ya kadi za njano na nyekundu kwa Makocha EPL 2018/2019
Kadi nyekundu na za manjano zitakuwa zikitolewa kwa mameneja na makocha kwa utovu wa nidhamu katika msimu huu
Mameneja (Makocha) wa Ligi ya Primia wataanza kupewa onyo la maneno kwa ” mienendo mibaya ” katika kampeni iliyoanzishwa ya 2018-19.
Tetesi za usajili barani Ulaya 1.8.2018
Lakini katika kombe la FA , Ligi ya soka, kombe la EFL na Ligi ya Taifa (NL) wataonyeshwa kadi nyekundu.

Iwapo kocha atapewa onyo mara nyingi itamsababishia kusimamishwa mara kadhaa pamoja na kupigwa marufuku kushiriki mechi moja ambayo inaweza kumsababishia kushtakiwa walau kwa makosa 16 ya utovu wa nidhamu.
Awali , maafisa wa mchezo walikuwa na mamlaka ya kuwaonya tu maafisa kabla ya kuwarejesha kwenye viti vyao kwa matukio makubwa ya ukiukaji wa maadili.
Kadi zinaweza kutolewa kwa matendo yakiwemo yale ya matumizi ya lugha mbaya ama ishara mbaya dhidi ya maafisa wa mechi, kupiga teke ama kutuma chupa za maji, kupiga kofi hewani na kuonyesha kupunga hewani kadi bandia.