Simba watoa Tamko juu ya wachezaji ambao hawakutambulishwa Simba Day

Simba watoa Tamko juu ya wachezaji ambao hawakutambulishwa Simba Day

0

Simba watoa Tamko juu ya wachezaji ambao hawakutambulishwa Simba Day

Jumatano 8.8.2018 Klabu ya Simba ilikuwa ikitambulisha wachezaji wake na vitu vingine ikiwemo timu yao ya wanawake, Na Gazeti lao jipya huku pia shughuli ikihitimishwa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya ASANTE KOTOKO kutoka nchini Ghana.

Lakini wakati watu wengi wakiwa wanasubiri kama baadhi ya Nyota wao ambao hawakuwa na timu Uturuki lakini pia wakiwa bado wanamkataba na Simba kama watatambulishwa ama la.

Wakati wengi wakisubiria kuona hali hiyo ni kwamba kuna wachezaji takribani wanne hawakutambulishwa wakiwemo Juuko Murshid, Haruna Niyonzima, Emmanuel Mseja na Said Mohammed Nduda.

Upande wa NDUDA na MSEJA ambao wao ni raia wa Tanzania na Usajili kwa Wachezaji wa Ndani ushafungwa uongozi wa Klabu ya Simba kupitia kwa Kaimu mwenyekiti wa Klabu hiyo Salim Abdallah umesema kuwa bado ni wachezaji halali wa Simba na hawakutambulishwa sababu walishindwa kufika uwanjani kwasababu mbalimbali.

Huku akisisitiza kuwa bado ni wachezaji wao na walishindwa kuwaacha kutokana na zoezi la kuwapeleka kwa mkopo timu nyingine kushindikana mpaka dirisha la usajili linafungwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY