Tetesi za usajili barani ulaya 8.8.2018

Tetesi za usajili barani ulaya 8.8.2018

0

Tetesi za usajili barani ulaya 8.8.2018

Kiungo wa kati wa Machester United raia wa Ufaransa Paul Pogba amewaaambia wachezaji wenzake kuwa anataka kuhama Old Trafford na kujiunga na Barcelona.

United wamekosa kumsaini mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng. Mlinzi huyo Mjerumani alimpigia simu meneja wa United Jose Mourinho kumuambia kuwa ameshukuru kwa nia hiyo lakini hawezi akaelekea Machester. (Bild)

Hata hivyo Leicester City wameipa United Matumaini mapya ya kumsaini mlinzi raia wa England Harry Maguire, 25, baada ya kuwaweka kwenye ofa walininzi wawili. Raia wa Crotaia Filip Benkovic, 21 alifanyiwa uchunguzi wa kiafya kablaa ya makubaliano yake ya pauni milion 13.5 kutoka Dainamo Zagreb na mkataba wa paunia milioni 22.5 kwa mchezaji wa Freiburg raia wa Uturuki Caglar Soyuncu, 22, unakaribia. (Mirror)

 

Kipa wa Athletic Bilbao Kepa, ambaye anakaribia kujiunga na Chelsea kwa paunia milioni 71.5 nusura ajiunga na Real Madrid kwa pauni milioni 17.9. Mlinda lango huyo raia wa Uhispania atakuwa kipa ghali zaidi wakati atahamia huko Stamford Bridge. (Guardian)

Kepa anasafiri kwenda London kukamilisha kuhama kwake kwenda Chelsea hatua ambayo itamuongezea mshahara wake wa sasa wa euro milioni kwa mwaka. (AS)

 

Atachukua mahala pake Mblegiji Thibaut Courtois ambaye anaamini kuwa kukataa kwake kurejea Chelsea kufanya mazoezi kutalipwa na kuhamia Real Madrid. Klabu hiyo ya Uhispnaia unajiandaa kumruhusu kiungo wa kati raia wa Croatia Mateo Kovacic, 24, kuelekea Stanford Bridge kwa mkopo kama sehemu ya mkataba huo. (Daily Telegraph)

Courtois, 26, anakabiliwa na faini ya pauni 200,000 kutoka Chelsea kwa kutojiunga na mazoezi. (Daily Mail)

 

Tottenham walitoa ofa ya pauni milioni 25 kwa mchezaji za zamani raia wa England kikosi cha chini ya miaka 21 Jack Grealish, 22, siku ya Jumanne na wanasubiri jibu kutoka kwa Aston Villa. (Telegraph)

Everton wana uhakika wa kumsaini mlinzi wa Chelsea Mfaransa Kurt Zouma, 23, kwa mkopo. (Mirror)

Everton wametoa ofa ya pauni milioni 10 kumsaini kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse, 23. (Sun)

 

West Ham wanajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Roma Mfaransa Maxime Gonalos, 29, kwa pauni milioni 8.9. Golanos anawavuti Everton na Crystal Palace. (90min)

West Ham wakati huo huo wana matumaini ya kukamilisha makubaliano ya pauni milioni 5 kumsaini mshambuliaji wa Asenal raia wa Uhispania mwenye miaka 29 Lucas Pezer ndani ya saa 24 zinazokuja. (London Evening Standard)

 

Crystal Palace na Fulham wote wanamtaka mshambuliaji wa Swansea City na Ghana Jordan Ayew. Mchezaji huyo wa miaka 29 anatakataa kufanya mazoezi na timu yake.(Mirror)

Newcastle United wanapanga kumuachia mlinzi raia wa Morocco Achraf Lazaar, 26, na kiungo wa kati ria wa Senegal Henri Saivet. (Chronicle)

Mshambuliaji mpya wa Brighton raia wa Afrika Kusini Percy Tau, 24, anatarajiwa kupewa kwa mkopo kwa Royale Union Saint-Gilloise ambao wanacheza ligi ya pili ya Ubelgiji. (The Argus)

Kipa wa England Jack Butland atalazimika kubaki Stoke City kwa sababu kumsainiaatakayechukua mahala pake itakuwa vigumu kwa kuwa tarehe ya mwisho inakaribia, kwa mujibu wa meneja wa Potters Gary Rowett. (Sentinel)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY