Tetesi za usajili barani Ulaya leo 3.8.2018

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 3.8.2018

0

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 3.8.2018

Real Madrid wameweka tangazo la kiwango cha bei ya £670m kwa mchezaji wa miaka 32 wa kiungo cha kati wa timu ya Croatia -Luka Modric, aliyetajwa kama mchezaji bora wa Kombe la Dunia la 2018, kuizuwia Inter Milan kujaribu kumchukua. (Mirror)

Manchester United imeafiki masharti binafsi ya mlinzi wa Barcelona Yerry Mina, mwenye umri wa miaka 23, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia akisubiri klabu ziukubali mkataba . (Metro, via Mundo Deportivo)

Winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 25, amewaambia wachezaji katika timu yake kwamba yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anaweza kuwasilisha maombi ya kuhamia Chelsea. (Mirror)

Barcelona imekubali masharti binafsi ya mchezaji wa Bayern Munich Arturo Vidal, huku mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chile mwenye umri wa miaka 31- akitarajiwa kuigarimu timu hiyo ya Championi ya Uhispania £27m. (Guardian)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amejipanga kwa mazungumzo na mlinda lango Thibaut Courtois, huku Real Madrid wakiwa tayari kusaini mkataba na Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 26 . (Diario AS, via Star)

 

Chelsea wanamtaka mchezaji wa Real Madrid Mateo Kovacic baada ya mchezaji wa kiungo cha kati kuripotiwa kukataa kuhamia Manchester United kwasababu ya mtindo wa mchezo wa Jose Mourinho’ . (Express, via Calciomercato

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumtoa mshambuliaji wake kutoka Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, kwa Bayern Munich kama sehemu ya mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29. (Mirror)

 

Hata hivyo, taarifa kutoka Ujerumani zinasema kuwa Martial badala yake atatumika katika mkataba wa kubadilishwa na mchezaji wa klabu ya Bundesliga Jerome Boateng mwenye umri wa miaka 29-anayechezea safu ya ulinzi ya timu ya German. (Bild)

Bournemouth watatakiwa kutoa £30m ili kuwashawishi Levante kumtoa mchezaji wao safu ya kati wa Colombia Jefferson Lerma, mwenye umri wa miaka 23, baada ya the Cherries kuwa kukataliwa pendekezo lao. (Sun)

 

West Brom wameiambia Burnley kuwa watatakiwa kulipa dau la £20m ikiwa watakubali kumtoa mshambuliaji wa safu ya mashambulizi wa England Jay Rodriguez. (Guardian)

Burnley walikataliwa pendekezo lao la £11m Middlesbrough la kumnunua mchezaji wa safu ya ulinzi Muingereza Ben Gibson, huku Everton pia wakionyesha azma ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Northern Echo)

 

Mchezaji wa safu ya kati wa Stoke City, raia wa Uskochi Charlie Adam, mwenye umri wa miaka 32, anataka kurejea katika klabu yake ya kwanza ya Rangers kabla ya kustaafu. (Talksport)

Mchezaji wa Anderlecht anayechezea safu ya kati ya Ubelgiji Leander Dendoncker, mwenye umri wa miaka 23, amekataa kuhamia katika Ligi ya Primia , kwa kukataa Crystal Palace na Wolves kwa pamoja . (Sun)

Hata hivyo , Wolves wako tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ili kumuweka kibindoni mchezaji wa Middlesbrough na Winga wa Uhispania Adama Traore, mwenyeumri wa miaka 22. (Telegraph)

BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY