Timu iliyovunja rekodi ya Gor Mahia kutofungwa miezi 7 Kenya

Timu iliyovunja rekodi ya Gor Mahia kutofungwa miezi 7 Kenya

0

Timu iliyovunja rekodi ya Gor Mahia kutofungwa miezi 7 Kenya

Gor Mahia the K’ogalo unaweza ukawaita kwa jina hilo pia jana wamejikuta wakipokea kichapo cha kwanza kwenye ligi kuu ya Kenya mara baada ya Kukaa takribani miezi 7 bila Kufungwa kwenye Ligi hiyo ya Kenya Sportpesa Premier League.

Kichapo ambacho Gor Mahia imekipata ni kutoka kwa wakali kutoka Mombasa timu ya Bandari ambao wakicheza katika uwanja wao wa Nyumbani wamewashushia Gor Mahia kichapo cha bao 2 kwa 1.

Mpaka Kipindi cha KWANZA kinamalizika Bandari Fc ilikuwa inaongoza kwa bao 2 kwa 0 na Kisha baadaye Gor Mahia wakapata bao la Kufutia machozi Kupitia kwa Jack Tuyisenge.

Bandari Fc baada ya Ushindi huo wanavunja rekodi ya miezi 7 ya Gor Mahia kutofungwa kwenye Ligi ya Kenya lakini pia wanawafunga baada ya mechi 22 za Msimu huu kucheza bila Kufungwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY