Uchambuzi: Hassan Dilunga anamiguu ya Dhahabu na Maamuzi kwa wakati

Uchambuzi: Hassan Dilunga anamiguu ya Dhahabu na Maamuzi kwa wakati

0

Uchambuzi: Hassan Dilunga anamiguu ya Dhahabu na Maamuzi kwa wakati

Simba msimu huu iliongeza nguvu kwa kusajili wachezaji kadhaa kutoka ndani na Nje ya nchi kwa lengo la kukifanya kikosi chao kuzidi kuwa Imara kwenye michuano ambayo kitashiriki.

Lakini katika maeneo ambayo ni wazi upinzani wa Namba ndani ya Kikosi cha Simba unaonekana kuwa Mkubwa ni kwenye kiungo mchezeshaji hapa naongelea namba 8.

Walikuwepo wachezaji kama Mzamiru Yassin, Said Ndemla na Haruna Niyonzima kwa msimu uliopita ambapo msimu huu wachezaji kama Cletous Chama na Hassan Dilunga wameongezeka kikosini na kufanya moto uzidi kuwaka.

Lakini msomaji wa kwataunit.co.ke wazungu  wanamsemo mmoja wanasema Numbers Don’t Lie wakimaanisha Namba huwa hazidanganyi.

Ni wazi katika viungo hawa mpaka sasa katika viungo hawa kwa wale waliopata nafasi ya Kucheza mchezaji Hassan Dilunga amewafunika wenzake kitakwimu chanya zaidi kwenye timu.

Katika mechi alizocheza mbili za Mwisho kati ya Arusha United na ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Hassan Dilunga ameonyesha utofauti mkubwa sana anapocheza eneo la Kati ya uwanja kama kiungo mchezeshaji.

Katika dakika takribani 122 pekee Hassan Dilunga amehusika kwenye magoli yote manne ambayo Simba imefunga mechi mbili za Mwisho.

Arusha United vs Simba

Katika mchezo kati ya Arusha United na Simba ukiwa ni mchezo wa Kirafiki Dilunga alicheza kwa dakika 45 pekee lakini alifanikiwa kutoa pasi za Usaidizi mbili kwa Emmanuel Okwi dakika ya 6 ya Mchezo na dakika ya 30 ya Mchezo.

Simba vs Mtibwa Sugar ngao ya jamii 2018

Akicheza na waajiri wake wa zamani Hassan Dilunga licha ya kucheza katika kiwango kikubwa bado alifanikiwa kuhusika tena kwenye mabao yote mawili ya Simba.

Bao la kwanza akitoa Assist kwa Meddie Kagere ambaye ilibidi apambane haswa mpaka anafunga lakini bao la pili katika mchezo ho Hassan Dilunga alifanikiwa kufunga mwenyewe kisha kuwaomba msamaha waajiri wake MTibwa Sugar.

Miguu ya dhahabu na Uharaka wa Matendo.

Ukiachana na Kuwa na uwezo wa kukokota na Kumiliki Mpira anapokuwa uwanjani lakini bado Hassan Dilunga amekuwa anamacho yanayoona kwa wepesi, Miguu yenye uwezo wa kupenyeza mipira katikati ya walinzi wa timu pinzani na kufika kwa washambuliaji wake.

Ndiyo maana nathubutu kusema Anamiguu ya Dhahabu na lakini pia maamuzi ya haraka na kwa wakati sahihi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY