Wachezaji 7 watakaokosekana Rayon Sports vs Yanga jumatano hii

Wachezaji 7 watakaokosekana Rayon Sports vs Yanga jumatano hii

0

Wachezaji 7 watakaokosekana Rayon Sports vs Yanga jumatano hii

Jumatano wiki Hii kutakuwa na mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Rayon Sports kutoka Kigali Rwanda dhidi ya Yanga mabingwa wa Kihistoria wa Ligi kuu ya Tanzania Bara wakitwaa mara 27.

Kuelekea mchezo huo msomaji wa kwataunit.co.ke Jumla ya wachezaji 7 watakosekana kuelekea mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali huku Rayon Sports wakiwa na wachezaji watano watakokosekana na Yanga ikiwakosa wachezaji wawili.

Wachezaji watano wa Rayon Sports watakaokosekana ni Kipa wao namba moja Kassim Ndayisnenga, Yannick Mukunzi na Mbondi Christ hawa wakiwa walifungiwa na CAF kutokana na kuonekana kuchochea vurugu kwenye mechi ya marudiano dhidi ya USM Alger huko nchini Algeria.

Wachezaji wengine ni Manzi Thiery na Niyonzima Olivier Seif ambao wanakabiliwa na Kadi mbili za njano kwahiyo wataukosa mchezo huo na kukamilisha idadi ya wachezaji watano ambao wataikosa Yanga Jumatano 29.8.2018.

Nao Yanga kupitia kwa meneja wake Hafidh Saleh amethibitisha kukosekana kwa wachezaji Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao wanakabiliwa na majeraha.

Yanga hawana cha kupoteza sana zaidi ya Kutaka kupata pesa nyingi zaidi za CAF kwani hata ikishinda hawatakuwa na nafasi ya Kufuzu wakati Rayon Sports wao wakishinda mchezo huo watasubiri matokeo kati ya USM Alger dhidi ya Gor Mahia. Kuzipata habari za Yanga kwa wakati Like Ukurasa wetu wa Facebook HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY