Yanga kumuaga Cannavaro zaidi ya Mechi 1 Mikoa Hii yatajwa

Yanga kumuaga Cannavaro zaidi ya Mechi 1 Mikoa Hii yatajwa

0

Yanga kumuaga Cannavaro zaidi ya Mechi 1 Mikoa Hii yatajwa

Wakati Yanga ikiwa tayari mkoani Morogoro kwaajili ya Kambi ya wiki mbili leo ndiyo siku rasmi ambayo itaanza mazoezi rasmi mkoani Humo baada ya jana kufika mkoani Morogoro salama salmin.

Yanga tarehe 12.8.2018 itacheza mchezo maalumu wa Kumuaga mchezaji na nahodha wao wa muda mrefu Nadir Haroub Cannavaro ikiwa mkoani Morogoro.

Lakini mwenyekiti wa kamati ya Mashindano klabu ya Yanga Hussein Nyika amesema kuwa yanga itafanya zoezi la Kumuaga nahodha wao wa zamani ambaye kwasasa ni meneja wa timu hiyo Nadir Haroub Cannavaro kwenye maeneo mengi nchini.

Kwamujibu wa Hussein Nyika amesema kuwa mpaka sasa mikoa kama Mwanza, Arusha imeshatuma maombi ya Kumuaga Nahodha Nadir Haroub Cannavaro na pia hata Zanzibar nao wamefanya Hivyo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY