Yondani aulizwa uwezo wa Kagere amtaja Mavugo

Yondani aulizwa uwezo wa Kagere amtaja Mavugo

0

Yondani aulizwa uwezo wa Kagere amtaja Mavugo

Ukiuliza moja ya walinzi bora kabisa nchini Tanzania kwa miaka ya sasa basi Mlinzi wa Yanga Kelvin Yondani ni moja kati ya mabeki bora wa kati nchini kwa miaka mingi sasa kwa wachezaji ambao alicheza nao na anaoendelea kucheza nao.

Beki huyo wa kati wa Yanga ameuliza kuhusu uwezo wa Straika wa Simba Mrwanda mwenye asili ya Uganda Meddie Kagere na Yondani kufunguka kuwa mchezaji huyo ni wa kawaida na yeye hamhofii.

Katika majibu ya Yondani ambaye alizungumza na Gazeti la Bingwa alifunguka kuwa hamhofii Kagere na watu wakitaka kuhakikisha hilo basi wasubiri watakapokutana kwani hata mshambuliaji wao wa zamani Laudit Mavugo naye alikuja kwa mbwembwe kama Kagere lakini akashindwa kufanya kama ambavyo wengi walitarajia.

Kelvin Yondani msomaji wa Kwataunit.co.ke alisema  anajivunia zaidi kucheza na wachezaji wakubwa washambuliaji wenye uzoefu mkubwa kwenye mechi za kimataifa Hivyo hana kabisa hofu na mchezaji huyo Meddie Kagere.

Simba na Yanga zitakutana September 30 katika uwanja wa Taifa mechi ambayo kwa mara ya kwanza kikosi cha Yanga kitakutana na Simba kwa msimu wa 2018/2019.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY