AFC Leopards yacheza mechi na Wafungwa wa gereza la kamiti

AFC Leopards yacheza mechi na Wafungwa wa gereza la kamiti

0

AFC Leopards yacheza mechi na Wafungwa wa gereza la kamiti

AFC Leopards waite Ingwe jana wameweka historia nyingine nchini Kenya kwa kucheza mechi na wafungwa wa Kamiti katika mchezo ambao ulikuwa maalumu kwaajili ya Uzinduzi wa mashindano ya ndani ya ligi ya wafungwa wa gereza la Kamiti.

Katika mchezo huo ambao ulihusisha wachezaji 7  kwa timu moja  badala ya 11 kama ambavyo imezoeleka ulichezwa ndani ya gereza na kushuhudiwa na Wafungwa huku AFC Leopards wakibanwa kwa sare ya bao 3 kwa 3.

Ikumbukwe Jumamosi hii AFC Leopards watacheza mchezo mwingine wa Kirafiki na klabu ya Simba  ambao ni mabingwa wa soka nchini na kisha Jumapili  9 September 2018 watacheza na Azam Fc katika mchezo wa Kirafiki.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY