Beki Mtibwa ataja kati ya Kagere na Makambo yupi Hatari

Beki Mtibwa ataja kati ya Kagere na Makambo yupi Hatari

0

Beki Mtibwa ataja kati ya Kagere na Makambo yupi Hatari

Wakati washabiki wengi wa soka wakiwa kwenye ushindani na Ubishani wa nani hatari wa kupachikia mabao nyavu kati Ya Mnyarwanda Meddie Kagere wa Simba na Mkongo Heritier Makambo wa Yanga

Beki wa kati wa Mtibwa Sugar Casian Ponera  msomaji wa kwataunit.co.ke amefunguka aonavyo yeye mwenye makali zaidi kati yao akimgusia na Emmanuel Okwi ndani yake.

“Kwangu mimi namuona Makambo kuwa ni bora  zaidi, nasema hivyo kwa sababu ana kila kitu anachotakiwa kuwa nacho mshambuliaji, ana nguvu, kasi, uwezo wa kumiliki mpira, anajua kupiga chenga lakini pia siyo muoga wa kupambana na mabeki wakorofi. “Okwi yeye ni mzuri, ana kasi na anajua kumiliki mpira lakini hana nguvu pia ni muoga wakati Kagere yeye siyo muoga, ana nguvu, kasi na uwezo wa kupambana lakini siyo mzuri sana katika kumiliki mpira na kupiga chenga, kwa hiyo Makambo yupo vizuri,” alisema Ponela.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY