Beki wa Rayon aliyemtuliza Makambo anatua Yanga

Beki wa Rayon aliyemtuliza Makambo anatua Yanga

0

Beki wa Rayon aliyemtuliza Makambo anatua Yanga

Kumbe Yanga hawakwenda nchini Rwanda kucheza na Rayon Sports pekee badala yake walienda pia kwa lengo la Kuangalia mashine ambazo zinaweza zikawafaa kwenye kikosi cha timu nyao.

Yes ndivyo unaweza ukasema kwani baada ya kupagawa na uwezo wa mchezaji Abdul Rwatubyaye ambaye ni beki wa kati aliyeweza kudhibiti vyema machachari ya Straika mpya wa Yanga Makambo kwenye mchezo huo

Related image

Lakini pia hata alivyoingia Yusuph Mhilu bado alionekana kuwamudu kwa kila kitu washambuliaji wa Yanga kwa kuwapora kikatili mpira lakini pia kuwadhibiti kwa kila namna

mwenyekiti wa kamati ya Usajili klabu ya Yanga Hussein Nyika hakutaka kuacha yapite hivihivi kwani baada ya mchezo huo alikutana na mchezaji huyo na kuyajenga ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawasiliano ambapo inaelezwa mchezaji huyo huenda akatua Yanga siku zijazo.

Hali hiyo inakuja ikiwa ni toka kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera afunguke kuwa anahitaji beki wa kati mwenye uwezo kama wa Yondani au zaidi lakini pia beki wa Kulia na Straika mmoja wa Kumsaidia Makambo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY