Erasto Nyoni anogewa na Kuifunga Yanga afunguka haya

Erasto Nyoni anogewa na Kuifunga Yanga afunguka haya

0

Erasto Nyoni anogewa na Kuifunga Yanga afunguka haya

ERASTO Nyoni wa Simba ndiye mchezaji wa mwisho kuifunga Yanga kwenye mchezo uliopita lakini ameapa tena ni lazima aifunge tena Yanga bao lingine kwa kichwa na kuipa pointi tatu timu yake.

 

Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mchezo huo namba 72 wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa kesho Uwanja wa Taifa saa 11:00 jioni.

 

Nyoni alifunga bao hilo kwa kichwa na kuipa Simba ushindi wa bao 1-0 msimu uliopita akiunganisha mpira wa faulo jirani na eneo la kona uliopigwa na Shiza Kichuya.

 

Beki huyo kiraka alisema: “Maandalizi yapo vizuri na nikipata nafasi tena ya kuitumikia timu yangu nitawafunga Yanga bao kama lile la kichwa nalikumbuka na nitafurahi sana tukifaniki­wa kupata pointi tatu muhimu.

 

“Natam­bua kwamba ushindani ni mkubwa hivyo mashabiki waendelee kutuombea, na­kumbuka msimu uliopita nilifaniki­wa kuipa pointi tatu timu yangu kwa bao la kichwa uwanja wa taifa, hivyo ni maombi yangu pia tuweze kushinda katika mchezo wetu, mashabiki waendelee kutuombea.”

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY