Gor Mahia mambo magumu wachezaji wanne watajwa Simba na Yanga

Gor Mahia mambo magumu wachezaji wanne watajwa Simba na Yanga

0
Gor Mahia mambo magumu wachezaji wanne watajwa Simba na Yanga
Wakati Gor Mahia ikisifika kwa siku za karibuni kwa kuvinyanyasa vilabu vingi vya Afrika Mashariki zikiwemo Simba na Yanga hali ndani ya klabu hiyo inaelezwa kuwa siyo nzuri kifedha na kumekuwa hakuna raha kwa wachezaji.
Hali hiyo inatokana na kutolipwa Mishahara na hela ya Posho kwa ushindi wa mechi 8 za Ligi kuu soka ya Kenya KPL inayodhaminiwa na Sportpesa.
Kutoka chanzo cha Ndani cha Timu hiyo inaelezwa wachezaji wanne mpaka sasa wameomba kuondoka mwishoni mwa Msimu akiwemo nahodha wa timu hiyo Harun Shakava.
Kumekuwa na mgomo baridi ndani ya timu hiyo kiasi cha kupoteza mechi nne mfululizo zikiwemo tatu za Ligi kuu ya Kenya KPL juzi wakikubali kichapo kutoka kwa Ulinzi Stars bao 2 kwa 0.
Wachezaji wengine walioomba kuachana na Gor Mahia na tetesi kuanza kutaja kuwa huenda wakaibukia Tanzania katika vilabu vya Simba na Yanga wakati wa Dirisha dogo ni MLINZI Charles Momanyi, Na Viungo Francis Kahata na Humphrey Mieno.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY