Gor Mahia wasisitiza hawajalipwa na Kaizer chief hela za Walusimbi

Gor Mahia wasisitiza hawajalipwa na Kaizer chief hela za Walusimbi

0

Gor Mahia wasisitiza hawajalipwa na Kaizer chief hela za Walusimbi

Nairobi Kenya.

Wakati kukiwa na kelele nyingi nchini Hapa Kenya juu ya hela ya Usajili ya aliyekuwa mlinzi wa kutumainiwa wa Gor Mahia Godfrey Walusimbi ambaye alisajiliwa siku kadhaa zilizopita na klabu ya Kazier Chief ya Afrika Kusini Uongozi wa Gor Mahia umeibuka na kusema bado hawajalipwa chochote na Klabu hiyo.

Uongozi wa klabu ya Gor Mahia kupitia kwa mwenyekiti wake Ambrose Rachier umeuthibitishia kwataunit.co.ke kuwa hela ya Usajili wa Godfrey Walusimbi bado haijatoka.

Ambrose alisema makubaliano yalikuwa walipwe kwa awamu mbili awamu ya kwanza mwezi wa nane na wamu ya pili mwezi wa kwanza mwakani lakini mambo hajaenda kama ilivyotegemewa kwani hata hela ya mwezi wa nane bado hawajalipwa.

29 August 2018 ilitangazwa rasmi na klabu ya Kaizer Chief kuwa Godfrey Walusimbi 29, kuwa ni mchezaji wao kwa mkataba wa miaka 3 kuitumikia klabu hiyo huku dau la usajjili likitajwa kuwa shilingi za Kikenya zaidi ya Milioni 7

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY