GorMahia na Leopards katika bato usajili wa Mchezaji wa Rayon

GorMahia na Leopards katika bato usajili wa Mchezaji wa Rayon

0

GorMahia na Leopards katika bato usajili wa Mchezaji wa Rayon

Nairobi Kenya.

Wapinzani wa jadi wa soka la Kenya timu za AFC Leopards na Gor Mahia wameingia katika ushindani wa mchezaji kutoka nchini Rwanda  anayecheza katika klabu ya Rayon Sports.

Mchezaji huyo ni Eric Rutanga ambaye anacheza nafasi ya Mlinzi wa Kushoto, Bato imekuja mara baada ya AFC Leopards kuanza mazungumzo na mchezaji huyo ambaye awali aliwahi kuhitajika katika klabu ya Gor Mahia.

Image result for eric rutanga

Eric Rutanga ambaye alifanya vizuri zaidi kwenye mchezo kati ya Gor Mahia na Rayon hatua ya makaundi kombe la Shirikisho Rayon wakishinda Ugenini mbele ya Gor kiasi cha kuwafanya Gor Mahia kumtamani beki huyo.

Lakini Gor Mahia  msomaji wa Kwataunit.co.ke wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kumsaini kutokana na kuondokewa na mchezaji wake Godfrey Walusimbi aliyejiunga na Kazier Chief mwezi uliopita lakini pia mchezaji huyo amewahi kukaririwa akisema anapenda zaidi kucheza Gor Mahia kwani ni klabu kubwa yenye wachezaji bora.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY