Habari njema na muhimu kutoka Yanga leo 4.9.2018

Habari njema na muhimu kutoka Yanga leo 4.9.2018

0

Habari njema na muhimu kutoka Yanga leo 4.9.2018

Baada ya hofu ya majeruhi kutanda kwenye kikosi cha Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL Yanga hali inaelezwa kuanza kuwa tofauti.

Straika tegemeo zaidi kwa Yanga msimu Huu Heritier Makambo ambaye awali ilielezwa angeweza kukaa nje kwa wiki mbili kutokana na maumivu aliyoyapata wakati wa mchezo kati ya Rayon Sports na Yanga tayari ameanza mazoezi na wenzake toka jana

Wakati huo huo mratibu wa klabu ya Yanga Hafidh Saleh ameiambia kwataunit.co.ke kuwa wachezaji wengine waliokuwa majeruhi Juma Mahadhi na Juma Abdul huenda leo au kesho wakaanza mazoezi na wenzao wanaofanya mazoezi katika uwanja wa Polisi Kurasini kujiandaa na mchezo unaofuata wa Ligi dhidi ya Stand United.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY