Hivi ndivyo Zahera alivyoponda aina ya Uchezaji wa Tshishimbi

Hivi ndivyo Zahera alivyoponda aina ya Uchezaji wa Tshishimbi

0

Hivi ndivyo Zahera alivyoponda aina ya Uchezaji wa Tshishimbi

Wakati washabiki wa Yanga wakiwa na Furaha kutokana na ujio wa Feisal Salum katika eneo la kiungo cha Yanga , Aliyekuwa akicheza mara nyingi katika nafasi hiyo msimu uliopita Papy Tshishimbi ameanza kuonekana siyo lolote sana katika mechi kadhaa za msimu huu.

Mpaka sasa Yanga imeshacheza mechi 3 za Ligi kuu lakini watu wengi wamekuwa wakiona kuwa Tshishimbi huyu siyo yule wa msimu uliopita

Kama ulifikiri ni watu hao tu wanaoona basi sahau kwani hata kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameona kuwa Tshishimbi hayuko sawa na baada ya mchezo kati ya Yanga na Coastal Union Mwinyi Zahera alifunguka mengi akiponda aina ya Uchezaji wake.

“ Tshishimbi anachoka uwanjani na kupwaya kwa sababu hana nidhamu ya mchezo. Anakwenda kila mpira ulipo kitu ambacho kinamfanya atumie nguvu nyingi na kutoka katika mfumo. Anatakiwa kutawanya mipira , kukaba na kuijenga timu kati sio kwenda mbele na nyuma , kulia na kushoto “ alisema Zahera

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY