Huyu ndiye mchezaji alitokea mazoezini leo Simba toka msimu uanze

Huyu ndiye mchezaji alitokea mazoezini leo Simba toka msimu uanze

0

Huyu ndiye mchezaji alitokea mazoezini leo Simba toka msimu uanze

Unakumbuka Utata ulioibuka Simba baada ya kusajili makipa wengi huku baadhi ya makipa wakiwa haijulikani hatma yao ndani ya Kikosi cha SImba licha ya kuwa bado wanamikataba?

Msimu uliopita Simba ilikuwa na Makipa Aishi Manula, Said Mohammed Nduda, Ally Salim na Emmanuel Mseja na Msimu huu wakamuongeza Deogratius Munishi Dida ambaye alikamilisha idadi ya makipa watano wa Simba.’

Kumbuka pia toka msimu huu uanze magolikipa ambao wamekuwa wakifanya mazoezi na Simba ni Aishi Manula, Ally Salim na Deo Munishi Dida wakati Mseja na Nduda wakiwa hawajulikani walipo.

Sasa leo msomaji wa Kwataunit.co.ke golikipa Said Mohammed Nduda kwa mara ya kwanza msimu huu ameonekana mazoezini katika mazoezi ya Simba yanayoendelea uwanja wa Gymkana jijini Dar Es Salaam akijumuika na wenzake wanaoendelea na mazoezi ya Kila siku.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY