Kocha Simba ataja mshambuliaji wake bora zaidi

Kocha Simba ataja mshambuliaji wake bora zaidi

0

Kocha Simba ataja mshambuliaji wake bora zaidi

Kocha wa Simba Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka kuhusiana na Straika anayemuona kuwa ni hatari zaidi ndani ya Simba na kwenye ligi kuu Tanzania Bara TPL

Kocha huyo amemwangia sifa Straika wake Meddie Kagere kutokana na uwezo wake mkubwa wa Kutimiza majukumu anapokuwa uwanjani.

“Sioni haja ya kuongelea mchezaji mmojammoja lakini kwangu naona Kagere ni mchezaji mzuri zaidi kwa kuwa amekuwa akitimiza maju­kumu yake ya kufunga na kuonye­sha ubora wake vizuri tofauti na washambuliaji wengine.

 

“Naona anafanya kazi kubwa kutokana na jukumu ambalo analo, timu yote inamtegemea kuweza kuleta ushindi na ndiyo maana nasema ni bora zaidi kwa kuwa yeye kazi yake ni ku­hakikisha anafunga mabao.

 

“Kuhusu Makambo, namjua kwa sababu ni mchezaji mwenye miguu miwili hawezi kumfikia Kagere,” alisema Aussems.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY