Kocha wa AFC Leopards awaaga wachezaji wake

Kocha wa AFC Leopards awaaga wachezaji wake

0

Kocha wa AFC Leopards awaaga wachezaji wake

Nairobi Kenya

Mambo yamezidi kuwa magumu upande wa AFC Leopards baada ya kocha wake wa Sasa Mu-Argentina Rodolfo Zapata kuwaaga wachezaji wake baada ya kupoteza mchezo wa Jumapili dhidi ya Sofapaka.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya AFC Leopards umefunguka kuwa wao hawajamfukuza kocha huyo lakini pia hawajapokea barua ya kujiuzulu lakini wao kama viongozi wako Tayari kwa maamuzi yoyote atakayochukua.

MRITHI WAKE AANZA KUTAJWA.

Inaelezwa kuwa kocha wa Nakumatt Melis Medo ndiye anaymendewa na mabingwa hao wa zamani wa Kenya AFC Leopards endpo kocha wao wa sasa Rodolfo Zapata ataamua kuvunja mkataba.

Kocha Rodolfo Zapata alijiunga na Leopards mwezi May mwaka huu akitokea Gaborone United ya Botswana na inaelezwa kuwa amebakiza mkataba wa miezi sita.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY