Maoni ya Zahera baada ya Aussems kupondwa Makopo na Washabiki

Maoni ya Zahera baada ya Aussems kupondwa Makopo na Washabiki

0

Maoni ya Zahera baada ya Aussems kupondwa Makopo na Washabiki

Mara baada ya mechi kati ya Mbao Fc na Simba kumalizika kwa Simba kufungwa bao 1 kwa 0 uwanja wa CCM KIRUMBA mengi sana yaliibuka ikiwemo baadhi ya viongozi kuzomewa na kufanyiwa Tafrani mbalimbali.

Lakini suala hilo halikuishia kwa baadhi ya viongozi wa Simba kwani hata kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems raia wa Ubelgiji huyu alikumbana na kadhaa ya kupondwa na makopo na baadhi ya washabiki ambao hawakuridhishwa na matokeo hayo ya Simba.

Baada ya tukio hilo kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye anakiri kuwa aliona video ya Kocha Mwenzake Patrick Aussems akifanyiwa tukio hilo na papa Zahera amefunguka kuwa hajapenda tukio hilo.

Zahera alifunguka kuwa siyo jambo zuri walilolifanya washabiki kwani ligi bado mbichi lakini pia mpira unamatokeo matatu, Kushinda , kushindwa au kutoa sare hivyo hakukuwa na sababu za washabiki kufanya kitendo kile.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY