Matokeo Mwadui Fc vs Azam Fc TPL Leo 14.9.2018

Matokeo Mwadui Fc vs Azam Fc TPL Leo 14.9.2018

0

Matokeo Mwadui Fc vs Azam Fc TPL Leo 14.9.2018

Fatilia matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Mwadui Fc ambao wapo nyumbani kuwakaribisha Azam Fc kutoka Dar Es Salaam.

mECHI iMEANZA

Mwadui 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya 2 ya Mchezo Mwadui wanakuwa wa kwanza kupata kona katika mchezo wa Leo, inapigwa kona lakini inakosa madhara kwa Azam Fc

Dakika 10

Mwadui Fc 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya 10 Kona ya Pili Mwadui Fc wanaipata, inapigwa vizuri inazaa kona nyingine ambayo golikipa Razack Abarola anaidaka

Dakika 15

Mwadui Fc 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya 19 Mwadui Wanapata bao mwamuzi wa Pembeni anaonyesha kuwa ni Offside

Dakia ya 24 Gerald Mathias anamjaribu Abarola , Ambaye anatema shuti lake na Kulidaka tena

Dakika ya 30

Mwadui Fc 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya 40 David Mwatika anapewa kadi ya njano baada ya kucheza rafu kwa mchezaji wa Mwadui

Mechi kati ya Mwadui Fc  na Azam Fc katika kipindi cha kwanza inamalizika kwa matokeo ya sare kwa 0 kwa 0.

HALF TIME

Mwadui Fc 0 – 0 Azam Fc

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha Pili Kimeanza

Mwadui Fc 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya 46 Nwadui wanaanza kwa kupata Kona

Dakika ya 50 Bado Mwadui 0 – 0 Azam Fc mechi ikiwa ni ya Kushambuliana kwa Zamu

Dakika ya 55 Goaaaaal Salum Abubakary Sure Boy anaipatia Azam Fc bao la Kuongoza kwa Shuti kali la chini chini Nje ya 18.

Mwadui 0 – 1 Azam Fc

Dakika ya 65

Mwadui Fc 0 – 1 Azam

Goaaaaaal dakika ya 71 Innocent Edwin anasawazisha bao kwa Mwadui Fc

Mwadui Fc 1 – 1 Azam Fc

TAKUKURU Yamsaka kiongozi wa Simba

Dakika 80

Timu zimekuwa zikishambuliana hapa na Pale timu zote zikipambana kuhakikisha zinapata bao la kuongoza licha ya Kuwa idara za Ulinzi kwa Mwadui na Azam Fc zimekuwa Imara kuhakikisha haziruhusu bao.

Mwadui 1 – 1 Azam Fc

Dakika ya 84 Azam wanapata Mpira wa Adhabu lakini Vipimo vya Aggrey Morisi vinazidi na Mpira Unapaa

Dakika 3 za Nyongeza katika uwanja wa Mwadui  bado 1 kwa 1

FULL TIME

Mwadui 1 – 1 Azam Fc (Salum Aboubakary Sure Boy, Inocent Edwin)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY