Matokeo Singida United vs Mbeya City leo 26.9.2018

Matokeo Singida United vs Mbeya City leo 26.9.2018

0

Matokeo Singida United vs Mbeya City leo 26.9.2018

Matokeo ya Moja kwa Moja ligi Kuu soka ya Tanzania Bara TPL Leo 26 September 2018 kutoka uwanja wa Namfua Mkoani Singida.

Mechi imeanza

Singida United 0 – 0 Mbeya City

Goaaaal Habib Haji Kiyombo anaipatia Singida United bao la kuongoza kwa mkwaju wa Penati

Singida 1 – 0 Mbeya City

Dakika ya 38 Makosa ya Tibar John Yanawakosesha Singida bao la Pili

Dakika ya 39 Iddi Nado aliwachekecha mabeki wa Singida United na Kuset Mpira kwa Eliud Ambokile lakini mpira alioupiga Ambokile unapita nje ya Lango

dAKIKA YA 40

sINGIDA united 1 – 0 Mbeya City

Zimeongezwa dakika 2 ili kuweza kuhitimisha dakika 45 za kipindi cha pili wakati ambao Singida United wakiwa wanaongoza kwa bao moja kwa sifuri

HALF TIME

Singida United 1 – 0 Mbeya City (23′ Habib Kyombo)

KIPINDI CHA PILI

Mechi Inaendelea kipindi cha pili

Singida 1 – 0 Mbeya City

Dakika ya 47 Mbeya City wanapata Kona baada ya kufanya shambulizi langoni mwa Singida United

Kona inshindwa kufanya maajabu yoyote na Singida wanaokoa

Dakika ya 55 Mbeya City wanapata Free Kick lakini mpira unaopigwa na Mapunda unagonga UKuta uliopangwa na Singida United

DAKIKA 60

Singida United 1 – 0 Mbeya City (23′ Habib Kyombo)

Dakika ya 61 Singida United wanafanya mabadiliko ya Kumtoa Kenny Ally na nafasi yake inachukuliwa na Awesu Awesu mchezaji wa zamani wa Madini ya Arusha na Mwadui Fc ya Shinyanga

Dakika ya 62 Singida United wanafanya mabadiliko mengine ya kumtoa Geofrey Mwashiuya na nafasi yake inachukuliwa na Eliuter Mpepo ambaye msimu uliopita alicheza Tanzania Prisons ya Mbeya

Dakika ya 64 Amara Diaby anapewa kadi ya njano kwa mchezo usio wa Kiungwana na ni Faulo kuelekea Singida United

Dakika ya 65 Eliuter Mpepo anajaribu shuti langoni mwa Mbeya City mpira unapita juu kidogo ya Lango.

Dakika ya 66 Samatta wa Mbeya City anatoka anaingia Seleman Ibrahim

Goaaaaal Dakika ya 67 John Tibaranapiga shuti nje ya 18 na kuipatia Singida United bao la pili.

Singida United 2 – 0 Mbeya City

dAKIKA 75

Singida United 2 – 0 Mbeya City (23′ Kyombo, 67′ Tibar)

Dakika ya 84 John Tibar mfungaji wa bao la pili la Singida anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Assad Juma

Dakika ya 89 Owen Chaima anafanya uzembe wa Ajabu unaoipa bao la 3 Singida United.

Singida United 3 – 0 Mbeya City

FULL TIME

Singida United 3 – 0 Mbeya City ( 23′ 67′ 89 Kyombo, Tibar, Kagoma)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY