Pawassa ataja mchezaji Yanga atakayewasumbua zaidi Simba Jumapili

Pawassa ataja mchezaji Yanga atakayewasumbua zaidi Simba Jumapili

0

Pawassa ataja mchezaji Yanga atakayewasumbua zaidi Simba Jumapili

Kuelekea pambano la watani wa Jadi Simba vs Yanga Jumapili 30.9.2018 katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam hakika mambo yameanza kuwa mengi na kila mtu akiongea lake.

Unamkumbuka yule beki kisiki aliyecheza kwa mafanikio ndani ya Simba Boniface Pawassa?

Basi kuelekea pambano la Simba na Yanga amekichungulia kikosi cha Yanga (Wapinzani wake wa zamani) na kusema kuwa kwasasa mchezaji wa Kuchungwa zaidi ndani ya Kikosi hiko ni Ibrahim Ajibu.

Pawassa alifunguka kuwa mchezaji huyo amekuwa na kiwango bora katika mechi za hivi karibuni kiasi cha kuwa ndiye chanzo cha mabao mengi ya Yanga hivyo Pawassa ametoa tahadhari kwa wachezaji wa Simba kuwa makini naye 30.9.2018.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY