Ratiba Ligi kuu Tanzania Bara TPL Leo 22.9.2018

Ratiba Ligi kuu Tanzania Bara TPL Leo 22.9.2018

0

Ratiba Ligi kuu Tanzania Bara TPL Leo 22.9.2018

Uhondo wa Ligi kuu soka ya Tanzania bara uanendelea leo Jumamosi 22.9.2018 katika nyasi za viwanja mbalimbali nchini Tanzania baada ya jana kushuhudiwa mchezo mmoja kati ya KMC ambao waliifunga bao 2 kwa 0 Stand United.

Leo Jumamosi Biashara United waliotoka kutoa sare ya bila kufungana na Azam Fc watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania kutoka Maeneo ya Mbweni Jijini Dar Es Salaam mechi ikichezwa katika uwanja wa Karume moja kati ya viwanja ambavyo vimekuwa vikijaza watu wengi katika mechi mbili za Biashara licha ya kutotoa ushindi kwa Biashara United.

Nao Ruvu Shootinga waite wazee wa Kupapaswa licha ya Kuanza ligi vibaya huku wao wakisingizia kukosa baadhi ya nyota wao ambao usajili wao bado unamadoa watakuwa nyumbani baada ya kuambulia kipigo kutoka kwa Mbeya City, Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Coastal Union uwanja wa Mabatini mechi itakayoanza saa nane mchana.

Alichosema Niyonzima baada ya taarifa ya Kuwapa Simba mechi 5 kama hatocheza kuvunja mkataba

Na mabingwa watetezi wa ligi Kuu TPL Simba watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Mwadui mechi ikichezwa Kambarage Shinyanga na itaanza saa kumi kamili alasiri.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY