Ratiba mechi 10 Ligi kuu Tanzania bara TPL wikiendi Hii

Ratiba mechi 10 Ligi kuu Tanzania bara TPL wikiendi Hii

0

Ratiba mechi 10 Ligi kuu Tanzania bara TPL wikiendi Hii

Ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL 2018/2019 Itaendelea kuanzia kesho siku ya Ijumaa mara baada ya mapumziko kupisha timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Uganda Kufuzu AFCON 2019.

Ratiba TPL Ijumaa 14.9.2018

Ijumaa Ligi kuu soka ya Tanzania bara itaendelea kwa mechi 2 kuchezwa,

Katika uwanja wa Mwadui wilayani Kishapu Mwadui Fc watakuwa wenyeji wa Azam Fc mechi ikianza saa nane mchana.

Nako Katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam AFrican Lyon watawakaribisha Coastal Union kutoka Tanga, Mechi Itaanza saa kumi alasiri.

RATIBA TPL JUMAMOSI 15.9.2018

Biashara ya Mara  msomaji wa Kwataunit.co.ke siku ya Jumamosi kwa mara ya kwanza watacheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi kuu katika uwanja wao wa Karume mkoani Mara mechi itakayochezwa dhidi ya Kagera Sugar.

KMC wao watakuwa wenyeji wa Singida United katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam saa kumi kamili alasiri.

Mbao Fc waranda bao kutoka mitaa ya sabasaba Ilemela jijini Mwanza watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba, Mechi Itaanza saa kumi kamili.

Nao wanajelajela Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani mechi ikianza saa kumi dimba la Sokoine Mbeya.

Lipuli Fc watakuwa nyumbani uwanja wa Samora kuwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar, Mechi hii Itaanza mapema saa nane mchana.

Mtwara kutakuwa na SHughuli kati ya Ndanda Fc dhidi ya Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba mechi itaanza saa kumi kamili.

RATIBA TPL JUMAPILI 16.9.2018

Mbeya City baada ya kupoteza mechi zake tatu za awali itakuwa nyumbani kwa mara ya kwanza toka msimu uanze kucheza na Alliance kutoka Mwanza , mechi ikianza saa nane mchana uwanja wa Sokoine.

Nao Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi kuu soka ya Tanzania bara Yanga watakuwa wenyeji wa Stand United chama la wana kuanzia majira ya saa kumi kamili uwanja wa Taifa kuanzia saa kumi kamili alasiri.

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY