Ratiba mechi 6 za Jumatano TPL 19.9.2018 Na muda

Ratiba mechi 6 za Jumatano TPL 19.9.2018 Na muda

0

Ratiba mechi 6 za Jumatano TPL 19.9.2018 Na muda

Ligi kuu soka ya Tanzania bara itaendelea jumatano hii kwa jumla ya mechi nne kuchezwa katika madimba SITA.

Mechi ya Mapema zaidi itakuwa kati ya Lipuli kutoka mkoani Iringa itakayoikaribisha Alliance Fc ya Mwanza uwanja wa Samora Iringa mechi ikianza saa nane mchana.

Mechi Nyingine itakuwa kati ya Ndanda na Mtibwa Sugar ikichezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara saa kumi kamili.

MWINYI ZAHERA ATIMUA WACHEZAJI WATATU KAMBINI YANGA

Mbeya City baada ya ushindi wa Kwanza TPL watakuwa nyumbani tena Sokoine kucheza na Ruvu Shooting mechi itaanza saa kumi kamili.

Mwadui wanaalmasi hawa kutoka wilayani Kishapu watakuwa nyumbani Mwadui Complex kucheza na JKT Tanzania wanaoongoza ligi kwa kuwa na Points 8, mechi saa kumi kamili.

RAMADHAN KABWILI AREJESHWA KIKOSINI YANGA

Biashara United ya Mkoani Mara watakuwa wenyeji katika uwanja wa Karume mkoani Mara kuwakaribisha Azam Fc kuanzia majira ya saa kumi kamili.

Na mechi ya Mwisho kwa siku ya Jumatano TPL Itakuwa kati ya Yanga ambao wataikaribisha timu ya Coastal Union kutoka Mkoani Tanga katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam mechi itakayoanza saa moja usiku.Kwa habari za Kila wakati kwa haraka Like Ukurasa wetu wa Facebook HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY