Simba wakata mzizi wa Fitna ishu ya Djuma na Aussems waamua hivi

Simba wakata mzizi wa Fitna ishu ya Djuma na Aussems waamua hivi

0

Simba wakata mzizi wa Fitna ishu ya Djuma na Aussems waamua hivi

Wakati hali ikionekana bado si shwari ndani ya klabu ya Simba kutokana na kocha kipenzi cha washabiki Masoud Djuma kutojumuishwa katika safari za mikoani na kocha mkuu Patrick Aussems Simba wamekuja na Tamko lao.

Simba kupitia kwa Msemaji wao Haji Manara akizungumza kwa kirefu leo kupitia kipindi cha Sports HQ cha EFM ametolea ufafanuzi mujarabu kabisa kuhusiana na Kinachhoendelea.

Haji manara msoamaji wa Kwataunit.co.ke amezungumza kuwa Makocha wengi ambao wamekuwa wakizifundisha timu kubwa za Tanzania kama Yanga na Simba wamekuwa wanapoondoka wanalalamika kuingiliwa katika majukumu yao na Viongozi.

Na hata washabiki wa Simba kwasasa wamekuwa ni kama wanataka kuingilia majukumu ya Kocha mkuu, haji amesema kwasasa wao wamemwachia kila kitu kocha Mkuu na hawataki kumwingilia katika maamuzi.

Ikiwa ni pamoja na hili la kumuacha Masoud Djuma kocha wake msaidizi kubaki na wachezaji wanaosalia Dar na mambo mengine ambayo amekuwa akiyafanya kama kocha Mkuu.

Haji Manara amemaliza kwa kusema bado Masoud Djuma ni kocha wa Simba na Uongozi utaendelea kuheshimu maamuzi ya Kocha Mkuu pasipo kumuingilia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY