Tetesi za Usajili barani Ulaya Jumamosi 29.9.2018

Tetesi za Usajili barani Ulaya Jumamosi 29.9.2018

0

Tetesi za Usajili barani Ulaya Jumamosi 29.9.2018

Baadhi ya wachezaji wa United wamekasirishwa na hatua ya Mourinho kuwakosoa hadharani walinzi Eric Bailly na Phil Jones baada ya kushindwa na Derby katika kombe la Carabao Jumanne hii. (Sun)

Ajenti wa Pogba, Mino Raiola, anatarajiwa kukutana na maafisa wa United mwezi Novemba kujadili hatima ya siku zijazo ya kiungo huyo wa kati. (Guardian)

Mourinho amemkemea mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 20, kwa kushindwa kupumzika vya kutosha baada ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Young Boys wiki iliyopita. (Mail)

 

Kiongo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas ,anaamini itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuendelea kumkwamilia Eden Hazard.

Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 27 alitaka kuondoka Stamford Bridge mwezi Julai lakini Chelsea ilisema haiko tayari kumuuza. (Evening Standard)

Kiungo mwenzake katika kilabu hiyo Ross Barkley amesema kwa sasa Hazard ni bora kuliko Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus Cristiano Ronaldo. (Guardian)

AC Milan imeonyesha nia ya kumnunua Fabregas, 31, na imesema kuwa iko tayari kujishindia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwezi Januari mwakani (Mundo Deportivo – kwa kihispania)

 

Kipa wa Everton kutoka Uingereza Jordan Pickford amesema tetesi zinazomhusisha na Chelsea msimu huu wa joto kamwe hazija athiri mipango yake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ametia saini kandarasi mpya na klabu ya Toffees siku ya Jumatano. (Sky Sports)

Manchester City inamtaka kiungo wa kati Tanguy Ndombele anayechezea Lyon na timu ya France ya wachezaji wa chini ya miaka 21.

Mchezaji huyo ametia saini kandarasi ya miaka mitano na Ligue 1 mwezi huu. (Le10Sport -kwa kifaransa)

 

Real Madrid imeweka dau ya beki Benjamin Pavard lakini Stuttgart imekataa.

Manchester United na Arsenal pia waliwahi kuonyesha nia ya kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (Sport Bild kipitia Metro)

West Ham imeboresha ofa yake kwa Declan Rice, 19, baada ya kiungo huyo kukataa ofa yake ya awali ya kima cha zaidi ya euro 40,000 kwa wiki. (Telegraph)

Newcastle imekataa kuzungumzia uwezakano wa kumtafuta mtu atakayemrithi meneja wake Rafael Benitez, ambaye kandarasi yake inakamilika mwezi juni mwakani.

Credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY